Wednesday, 23 November 2016
Kenya's Singing Cop Sammy Ondimu Ngare Calls Out Politicians For Their Duplicitous Statements About Corruption In The Force
Popular Kenyan cop Sammy Ondimu Ngare known for his social campaign #AskariNiBinadamu has written a strongly worded opinion piece about how politician treat their bodyguards.
This article was inspired by ulcerations by politicians who claimed the force is mered with rampant corruption and that they are paid for doing nothing.
In his opinion piece, Sammy, highlights the lifestyle of a mheshimiwa's bodyguard. He does this in a bid to shed light into the life of a man in the force. This is in line with his social campaign, #AskariNiBinadamu for Kenyan citizens to view policemen as human.
Here is his opinion piece on the matter.
KILIO CHANGU SAMMY (ASKARI) KWA MHESHIMIWA.
Ukisimama kwa podium unaongea mbaya kutuhusu.. "Ooh nyinyi ni wajinga, kazi yenu ni kupokea hongo tu, mnatumika vibaya, kazi imewashinda, tunawalipa mishahara bure na hamfanyi kazi..."
Imagine unapoongea haya yote niko nyuma yako kama mlinzi (bodyguard). Hebu fikiria naingia job mapema na kutoka late usiku wa manane.watoto wangu hawanijui maana natoka asubuhi na nikirudi washalala. Weekends hautaki niwe na familia yangu wataka nikupeleke kwenye starehe ujienjoy na wenzako. Mkutanapo kwenye starehe zenu sisi twabaki kwa magari tukinyosha viti tukilala tukisubiri simu zenu. Wala lunch ya 7k, pesa yatosha kulipia mtoi wangu shule. Dinner pekee yalipia rent familia yangu. Uingiapo kwako outside kuna colleague yuapigwa na baridi kukupa security. Hata haumjui kwa jina. Usiku usikiapo risasi zikilia wampigia simu na kutaka kujua ni nini mbaya. Nikichelewa kufika kazini asubuhi wapigia wadosi wangu na kuwaambia uwongo wote vile mimi ni mbaya.
Juzi nimewaona waheshimiwa kwa vyombo vya habari mkisema mtahamisha Askari wote toka kwa county, nashangaa wale mnataka wazuri watatoka wapi. Sijawahi kuona hata siku moja polisi twasifiwa kwa kazi njema tulofanya na sio eti hatufanyi. Hebu jiulize mhesh, uko na askari anakulinda usiku na mchana ushawahi take your time kujua yuaishi vipi? Anakula nini? Watoto wake wanasomea wapi?
Bungeni hautetei maslahi yangu, wajua mshahara wangu hata sio nusu ya entertainment allowance yako. Je, mheshimiwa wajua kuwa mimi ni mwanadamu kama wewe? Wewe ukiumia hata kama ni headache wabebwa na ndege hadi ngambo kwa matibabu zaidi, mimi hata hiyo ndege siijui vile inakaa ndani, sijui kama iko na steering, brake, clutch ama gears...huwa naiona tu kwa TV, gazeti na maybe nikikupeleka airport naona ikitake off.
#Askari_ni_Binadamu. Kama sio wewe mheshimiwa, Nani basi atatusaidia? Natumahi kilio changu utakisikia na utashugulikia maslahi yangu..
Kumbuka ukinitusi mimi ni mjinga, yule ako nyuma yako kama bodyguard sio eti ni tofauti na sisi.
Mola akulinde nami anilinde pia, tunapoendelea kuhudumia wakenya.
Mola aibariki Kenya yetu.
#AskariniBinadamu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment